Rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania(TFF) Wallace Karia amesema wamekuwa kimya kwa muda mrefu kwa kuhofia kuharibu mipango ambayo wanaendelea nayo lakini sasa wamefikia pazuri na muda wowote wanaweza kupata mdhamini mkuu wa ligi.
''Kuhusu mdhamini tumefikia pazuri, hivi karibuni tulikuwa mjini Durban Afrika Kusini, tumeongea na kampuni moja ambayo inafanya shughuli zake hapa nchini kwahiyo tupo kwenye hatu nzuri ya kupata mdhamini'', amesema Karia.
Karia amesema sababu za kujitoa mdhamini aliyekuwepo kampuni ya Vodacom ni kwasababu walishusha kiwango cha fedha na wao kama TFF hawakuwa tayari kuendelea nao kulingana na thamani ya ligi hivyo wakaachana.
Ligi kuu soka Tanzania bara ambayo ipo katika raundi ya 13 inaendelea bila kuwepo kwa mdhamini mkuu hivyo hata zawadi ya bingwa bado haijawekwa wazi.
Chanzo:Eatv
Social Plugin