Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAWILI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WAKIWAIBIA ABIRIA


Moja ya picha ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta

Wapelelezi wamefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao ni wafanyakazi wa kampuni inayotoa huduma za kupokea abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) nchini Kenya wakiiba pesa za abiria.

Watuhumiwa hao ambao ni Kennedy Ochieng, mwenye umri wa miaka 22 na Bw Kevin Ogega, mwenye umri wa miaka 25, ambao wote ni wanafanyakazi wa kampuni ya kubeba mizigo katika uwanja huo, wamedaiwa kuiba pesa za abiria baada ya kukutwa nazo kufuatia msako mkali.

Licha ya kupatikana kwa pesa hizo, Polisi nchini Kenya haijathibitisha ni wapi pesa hizo zimepatikana.

Matukio ya abiria kuibiwa pesa katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) yamekuwa yakiripotiwa mara kadhaa, ambapo mwezi Mei mwaka huu raia mmoja wa Iran aliyetambulika kwa jina la Mehrah Hassan ,30, aliripoti polisi kufuatia kuibiwa kiasi cha Dola za kimarekani 7,500 katika begi yake akiwasiri katika uwanja huo akitokea nchini Qatar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com