Idadi ya vifo iliyotokana na janga la kimbunga cha Tsunami kilichoikumba Indonesia inaendelea kuongezeka. Watu 373 wamethibitishwa kupoteza maisha na wengine 1,400 wamepata majeraha.
Kwa mujibu wa DW Swahili, Idadi hiyo ya vifo inategemewa kuongezeka zaidi, huku watu 128 wakiwa hawajulikani walipo hadi sasa hasa katika maeneo yaliyoathirika vibaya ya pwani ya kisiwa cha magharibi cha Java na kisiwa cha kusini cha Sumatra.
Juhudi za kutafuta miili ya mamia ya watu pamoja na kuwanusuru waliopata majeraha zimeongezeka leo hii kufuatia kimbuga cha Tsunami cha hivi karibuni kilichopiga nchini Indonesia. Wataalamu wamekusanya ushahidi unaothibitisha kwamba kimbunga hicho kilichochewa na mlipuko wa volkano.
Ni kwa mara ya pili kimbunga cha Tsunami kinapiga Indonesia ndani ya mwaka huu. Matetemeko makubwa ya ardhi yalichochea kimbunga hicho cha Tsunami na kupiga kisiwa cha Sulawesi mwezi Septemba.
Social Plugin