Klaus Kindoki (wa pili kulia) akiwa benchi na wachezaji wengine wa Yanga
Mlinda mlango namba mbili wa Yanga kwa sasa, Klaus Kindoki hatimaye ameondoa mkosi kwa kusimama golini hadi mpira unamalizika na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya African Lyon.
Kindoki ambaye amekalia benchi kwa kipindi kirefu tangu alipoharibu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya mwadui FC mjini Shinyanga mwezi uliopita, ameingia leo katika kipindi cha pili baada ya Ramadhani Kabwili kuumia na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Bao la Yanga limefungwa na Abdallah Haji Shaibu katika dakika ya 64 ya mchezo huo baada ya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa sare tasa.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga inafikisha pointi 47 katika michezo yake 17 iliyocheza mpaka sasa, huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote na kuzidi kuwakimbia wapinzani wake katika msimamo wa ligi, Azam FC iliyopo nafasi ya pili na Simba iliyopo nafasi ya tatu.
Chanzo - EATV