Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HIKI NDIYO KIWANDA KIKUBWA ZAIDI DUNIANI

Kiwanda hicho sasa kinaunda kizazi kipya cha ndege aina ya Boeing

Shirika la Boeing lilipoamua kuunda ndege yake chapa 747 - lilijizolea sifa kwa kufungua mlango wa kutengeneza ndege kubwa zaidi duniani.

Hata hivyo shirika hilo lililazimika kujenga kiwanda kikubwa zaidi ambacho kina uwezo wa kukidhi mahitaji ya ndege hiyo.

Ikiwa umewahi kuona ndege aina ya 747 ikiwa karibu, bila shaka utafahamu ukubwa wa ndege hiyo.

Kwa hivyo si ajabu kuona kiwanda kilichounda ndege hiyo kuishia kuwa na jumba kubwa zaidi la kiwanda.


Jengo kubwa kiasi gani?

Boeing ilianza kujenga kiwanda cha Everett mwaka 1967, muda mfupi baada ya mradi wake wa Boeing 747 kuanza kushika kasi.

Bill Allen, mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu katika kampuni ya Boeing, anasema shirika hilo lilifahamu fika kuwa, linahitaji sehemu kubwa, endapo lina mpango wa kuunda ndege ya kubeba abiria 400.

Waliamua kuchagua eneo la takriban kilomita 35 Kaskazini mwa jiji la Seattle, karibu na uwanja wa ndege ambao ulitumika kama kituo cha vita wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.

Ripoti katika jarida la Daily Herald liliangazia eneo hilo lililokuwa tu na barabara ndogo mno ya kufikia barabara kuu ya lami, na hakukuwa na njia ya reli kabisa kuunganisha eneo hilo, huku ukizungukwa na msitu ambao ulikuwa makao ya dubu, waliokuwa wakirandaranda humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com