Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUMBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA 4

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa majina ya Mmanga Mrope (47), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tunduru kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka minane, mtoto ambaye alikuwa akimlea. 

Wakati akisomewa mashtaka hayo, Desemba 14 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Abdalah Amwero, mwendesha mashtaka Inspekta Steven Msongaleli alidai kuwa kwa mara ya mwisho mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 6, mwaka huu, majira ya saa 4.40 usiku baada ya kumvamia na kumziba mdomo mtoto huyo na kufanikisha azima yake.

Msongaleli alidai kuwa mtuhumiwa huyo alianza tabia ya kumwingilia mtoto huyo anayesoma darasa la tatu (jina la shule linahifadhiwa) pamoja na kumfanyia kitendo hicho kinyume cha maumbile katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Alisema kwa kufanya hivyo Mrope alifanya kosa kinyume cha sheria namba 130 (1) na (2c) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 2002.

Mtuhumiwa huyo alibainika baada ya mtoto kumwambia mwalimu wake wa darasa baada ya kumhoji kutokana na mtoto huyo kuonekana kukosa furaha wakati wote anapokuwa shuleni, ambapo baada ya kubaini hivyo, walimu walimuhoji mtoto huyo na kuwaeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa akimtishia kumuua na kukimbilia nchi jirani ya Msumbiji endapo angetoa siri.

Mtoto huyo alipelekwa katika hospitali ya wilaya ya Tunduru kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na vipomo kuthibitisha iwapo alifanyiwa kitendo hicho. Mwendesha mashtaka amedai kuwa baada ya vipimo kubaini hivyo, ndipo mtuhumiwa alikamatwa.

Mtuhumiwa amekana kufanya kosa hilo na kupelekwa rumande baada ya kukosa wadhamini. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 18 kwa ajili ya kusikilizwa tena.
Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com