Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwalubambo.
Wanawake wanne (majina yamehifadhiwa) wakazi wa kijiji cha Buganzu kata ya Lunzewe Mashariki, Wilayani Bukombe Mkoani Geita wamebakwa na wanaume zaidi ya mmoja baada ya kuvamiwa na watu hao wakiwa majumbani mwao.
Tukio la kubakwa wanawake hao limetokea Desemba 11 majira ya saa nane usiku katika kijiji hicho, walipovamiwa na wanaume wanne wakiwa wamelala kisha kubakwa na kila mmoja na kupelekea kuwasababishia maumivu makali.
Akizungumza Mkoani Geita Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwalubambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watuhumiwa waliofanya unyama huo wamekwishakamatwa ambapo amewataja kuwa ni pamoja na George Deogratius(42) maarufu (Tolu) mkazi wa Ibamba, Josephat Emmanuel(25) mkazi wa Kabuhima, Rashid Maganga(18)) na Albert Makisio maarufu Kamkono wote wakazi wa Ibamba.
Kwa mjibu wa Kamanda Mponjoli, matukio mengine ni pamoja na watu wawili kuuawa Desemba 19 majira ya usiku, na wananchi wenye hasira kali wakiwa katika jaribio la kutenda uhalifu katika kijiji cha Nyakahengere kata ya Lukalanga Mjini Geita.
Social Plugin