Mwanamke aliyeokolewa na polisi baada ya kushikiliwa mateka kwa miaka 30 (wapili kushoto) na mwanae wa miaka tisa wameungana na familia yao.
Operesheni ya kumnasua mwanamke huyo ilifanyika kwa ushirikiano wa polisi wa nchi za Argentina na Bolivia.
Mahala ambapo alikuwa akishikiliwa mwanamke huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 45 lilikuwa halifahamiki toka miaka ya 80.
Hata hivyo, mapema mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa alikuwa akishikiliwa katika eneo la Bermejo, kusini mwa Bolivia baada ya uchunguzi, polisi walifanikiwa kuitambua nyumba aliyokuwemo na kufanikiwa kumuokoa akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa.
Katika taarifa iliyotolewa na polisi nchini Argentina wanasema mwanamke huyo amefanikiwa kurejeshwa na kuungana na familia yake katika mji wa Mar del Plata.
Taarifa hiyo hata hivyo haikusema ni nani aliyetekeleza tukio la utekaji miaka 32 iliyopita, huku pia jina la mwanamama huyo pamoja mtoto wake hayatajwa.
Chanzo: Bbc
Social Plugin