Wafanyabiashara wa Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya wamelazimika kufunga biashara zao kwa zaidi ya saa sita baada ya kuibuka vurugu za uchomaji mataili katika barabara ya mfikemo Mwanjelwa na kusababisha jeshi kuwafukuza wafanyabiashara wote katika Soko hilo.
Wakizungumza nje ya soko la Mwanjelwa, wafanyabiashara wa soko hilo wamelalamikia kitendo cha jeshi la polisi kuwafukuza na kusitisha biashara zao kwa saa kadhaa kutokana na vurugu za kuchoma matairi jirani na soko hilo.
Wafanyabiashara hao wamesema waliochoma mataili ni machinga kutoka nje na pamoja na hayo tayari jeshi la polisi limewatia mbaroni watu wawili wakidaiwa kuhusika na vurugu hizo.
Social Plugin