Suzana Magufuli ambaye ni mama mzazi wa Rais John Magufuli anaumwa ugonjwa wa kiharusi na anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Desemba 30, 2018 na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu imesema Rais Magufuli mara baada ya kutoka kanisani asubuhi alikokuwa akifanya ibada katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Parokia ya Oysterbay alikwenda kumjulia hali mama yake.
Rais Magufuli ameongoza maombi ya kumwombea mama yake pamoja na wagonjwa wote wanaokabiliwa na maradhi na kuwatakiwa heri ya mwaka mpya 2019.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Magufuli amewashukuru wauguzi wanaomhudumia mama yake na wagonjwa wengine nchini na kuwaombea kwa Mungu wapate heri na nafaka katika majukumu yao.
“Ee Mungu mwenyezi mwenye huruma, tunajua uko pamoja na mama yetu, umemsaidia katika kipindi cha zaidi ya miezi mitatu alipopata kiharusi, tunampenda lakini tunapitia katika upendo wa mwanao Yesu Kristo umjalie.
“Tunaingia katika mwaka mpya wa 2019 mama yetu apone, akaingie akiwa na afya njema, ukamsaidie katika tatizo lake aweze kupona.”
“Tunawaombea pia wagonjwa wengine wote katika nchi yetu ya Tanzania, ambao wanahangaika na matatizo mbalimbali, waliopo hospitalini, nyumbani Mungu Baba ukawashike waweze kupona.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Wasaidizi wake wakimuombea Mama yake Mzazi Bibi. Suzana Magufuli anayepatiwa Matibabu Jijini Dar es Salaam Desemba 30, 2018.
Bibi Suzana Magufuli anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ambapo amekuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miezi mitatu sasa.
Bibi Suzana Magufuli anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ambapo amekuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miezi mitatu sasa.
Social Plugin