Picha : WATUMISHI WA SERIKALI MAKADA WA CCM WAANDAMANA SHINYANGA KUFIKISHA UJUMBE KWA RAIS MAGUFULI



Watumishi wa serikali kutoka idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameandamana kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya ya kizalendo na kutetea wakulima kwa kupambana na wanyonyaji ambao wamekuwa wakitajirikia jasho lao na wao kubaki maskini.


Maandamano hayo yamefanyika leo Jumapili Desemba 2,2018 kutoka katika Soko Kuu la mjini Shinyanga hadi kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kufikisha ujumbe wao kwa Rais Magufuli za kuunga juhudi za utendaji wake kazi.

Akizungumza mara baada ya kumaliza maandamano hayo. Msemaji wa umoja huo wa watumishi wa Serikali ambao ni makada wa CCM Christopher Malengo,sambamba na kutoa tamko lao mbele ya katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa, amesema wameguswa na kazi ya kizalendo ambayo anaifanya Rais Magufuli ya kupigania maslahi ya wanyonge wakiwamo wakulima.

Amesema Rais Magufuli amekuwa akijikita katika misingi ya ujamaa,utu,uzalendo na haki kama alivyokuwa akifanya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye utawala wake, katika kuhakikisha anapigania maslahi ya wanyonge na kukomesha wanyonyaji ili wananchi wote waweze kupata haki sawa, vitendo ambavyo zinapaswa kupongezwa.

“Sisi kama watumishi wa serikali kutoka halmshauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni makada wa CCM, tumeamua kuungana kwa pamoja ili kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya ya kizalendo ya kupigania maslahi ya watanzania wote wakiwamo wakulima,” amesema Malengo.

“Tumeona mfano mzuri alioufanya kwenye zao la Korosho huko Mtwara amewapigania wakulima dhidi ya wanyonyaji pamoja na kuagiza zao hilo iuzwe kwa bei ya Shilingi 3,300 jambo ambalo ana stahili pongezi sana, na tunamuomba ageukie na mazao mengine likiwamo Kahawa na Pamba,”ameongeza.

Aidha amesema Sekta ya kilimo ndiyo injini ya mapinduzi ya viwanda, ambapo malighafi nyingi za uzalishaji bidhaa hutegemea mazao, hivyo jambo ambalo anafanya Rais ana paswa kuungwa mkono ili Tanzania tuweze kufikia uchumi wa kati mwaka 2025.

Kwa upande wake katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa amewapongeza watumishi hao wa Serikali kwa kutambua kazi anayofanya Rais Magufuli na kuwataka wasimwangushe bali waige mfano wake na kuchapa kazi kwa kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi.

TAZAMA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI

Watumshi wa Serikali katika idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni Makada wa Chama Cha Mapinduzi CCM wakiwa kwenye maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake mzuri wa kizalendo hasa kupigania maslahi ya wakulima,huku wakiwa wamebeba mabango ya pongezi hizo.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog

Maandamano yakiendelea kutoka eneo la Soko Kuu na kuelekea kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga ili kufikisha ujumbe wao wa pongezi kwa Rais Magufuli.

Maandamano yakiendelea sambamba na ubebaji wa mabango yenye Ujumbe wa pongezi kwa Rais John Magufuli.

Maandamano yakiendelea.

Maandamano baada ya kufika katika ofisi za CCM Mkoa wa Shinyanga.

Watumishi wa Serikali ambao ni Makada wa CCM wakifurahi mara baada ya maandamano hayo kupokelewa na katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa akipokea mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake kazi hasa kupigania wanyonge ili kuwainua kiuchumi.

Upokeaji wa mabango ukiendelea.

Watumishi wa Serikali ambao ni Makada wa CCM wakiingia ukumbini kwa ajili ya kutoa tamko lao juu ya kupongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake kazi wa kizalendo na kufuata misingi ya ujamaa, utu na uzalendo kama alivyokuwa akifanya hayati Baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye utawala wake.

Msemaji wa umoja huo wa watumishi wa Serikali kutoka halmshauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini ambao ni Makada wa CCM, Christopher Malengo akisoma Tamko la Pongezi kwa Rais Magufuli juu ya uchapakazi wake kazi wa dhamira ya kuinua uchumi wa nchi na kujenga miundombinu mbalimbali ikiwamo barabara,Reli ,kununua Ndege, pamoja na kupigania maslahi ya wakulima.

Wajumbe wakiwa ukumbini wakisikiliza uwasilishwaji wa Tamko lao kwa Rais John Magufuli..

Wajumbe wakiendelea kusikiliza kwa makini..

Wajumbe wakiwa ukumbini kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wakiwa ukumbini.

Msemaji wa umoja huo wa watumishi wa Serikali ambao ni Makada wa CCM Christopher Malengo akimkabidhi Tamko lao la Pongezi kwa Rais John Magufuli, katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwabwa, ili kuliwasilisha kwa Rais.

Muonekano wa nje wa Tamko hilo la Kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake kazi mzuri.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa, akiwapongeza watumishi hao wa Serikali ambao ni Makada wa CCM kwa kutambua kazi anayofanya Rais Magufuli, na kuwataka wasimwangushe bali waige mfano wake na kuchapa kazi kwa kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuwaahidi Tamko hilo litamfikia Rais John Magufuli.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم