Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari pamoja na watumishi wa wizara hiyo (hawapo pichani) baada ya kuingia mktaba na SUMA JKT wa ujenzi wa ofisi za wizara hiyo ambazo zitajengwa eneo la Ihumwa Jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof Adolf Mkenda kulia akibadilishana karatasi na Meneja wa Kanda kutoka SUMA JKT Meja Daudi Zengo baada ya kuingia mktaba wa ujenzi wa ofisi za wizara ya Maliasili na Utalii leo Ofisini kwake Jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof Adolf Mkenda akimshuhudia Mkurugenzi wa huduma za Sheria wa Wizara Bi.Venosa Mkwizu akiweka saini kutoka kushoto ni Meneja wa Kanda kutoka SUMA JKT,Meja Daudi Zengo hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Wizara hiyo Jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof Adolf Mkenda akimtazama Meneja wa Kanda Meja Daudi Zengo kutoka SUMA JKT akisaini Mktaba wa Ujenzi wa ofisi za Wizara hiyo ambazo zitajengwa eneo la Ihumwa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof Adolf Mkenda akiweka saini kushoto kwake ni Meneja wa Kanda Meja Daudi Zengo kutoka SUMA JKT akishuhudia mktaba huo wa ujenzi wa ofisi za Wizara hiyo ambazo zitajengwa Ihumwa jijini Dodoma
......................
Na Alex Sonna,Dodoma
Katika utekelezaji wa kuhakikisha Dodoma inakuwa Makao Makuu ya Nchi,SUMA JKT imeingia mkataba na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya Ujenzi wa ofisi za Wizara hiyo.
Mbali na kuingia mkataba na Wizara hiyo imeelezwa kuwa ujenzi huo utafanyika na kukamilika ndani ya mwezi mmoja.
Katibu Mkuu wa Wizra ya Maliasili na Utalii,Prof Adrof Mkenda akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa kutiliana mkataba wa ujenzi wa ofisi za Wizara ya Malisili na utalii ambazo zitajengwa na SUMA JKT alisema kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi mmoja.
Prof.Mkenda amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa agizo ra rais kutaka Dodoma kuwa makao makuu na Wizara zote kuhamia Dodoma kwa sasa Wizara ya Maliasili na Utalii imeamua kuingia mkataba na SUMA JKT kujenga ofisi za Wizara husika kwa kuzingatia kuwa SUMA JKT wanafanya kazi zao kwa viwango na kwa kuzingatia muda.
Aidha amesema ofisi hizo zitajengwa katika mji wa kiserikali ambapo eneo la ujenzi wa ofisi hizo zitakkuwa zimejengwa katika eneo la Ihumwa ndani ya jiji la Dodoma.
Prof.Mkenda amesema kuwa kwa kipindi ambacho watumishi wa serikali kupitia wizara hiyo ambao wamehamia Dodoma kwa sasa wanafanya kazi katika ofisi za wizara hiyo ambazo zipo ofisi ya barabara ya polisi na wengine wanafanya kazi wakiwa katika majengo ya Chuo kikuu cha Dodoma.
“Pamoja na kuwa kwa sasa tunafanya kazi bila kuwa na majengo ya kutosha lakini kazi zinafanyika vizuri na kwa ushirikiano mzuri huku wakiwa wanasubiria kupata ofisi ya uhakika ambayo itajengwa na Suma JKT katika mji wa kiserikali Ihumwa jijini hapa.
“Ninaamini kuwa iwapo tutakaa katika jengo moja la ofisi na watumishi kufanya kazi kwa pamoja tutafanikiwa kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri zaidi na wenye tija kwa manufaa ya taifa na jamii kwa ujumla ” amesema Prof .Mkenda.
Hata hivyo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo la ofisi litakamilika kwa muda mfupi kwa maana kuwa ujenzi huo utakuwa na awamu mbili ikiwa ujenzi wa awamu ya kwanza ni ujenzi wa jengo la awali na baadae litajengwa jengo kubwa ambapo wakurugenzi wote watakuwa wamehamia hapo.