Manchester United wametumia kifungu kwenye mkataba wa kipa wao David de Gea kinachowaruhusu kumuongezea mkataba kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja.
Wamechukua hatua hiyo kuondoa utata kuhusu mustakabali wake, dirisha ndogo la kuhama wachezaji litakapofunguliwa Januari.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alijiunga na United kutoka Atletico Madrid mwaka 2011.
Mkataba wa sasa wa De Gea, 28, unafika kikomo mwisho wa msimu, jambo ambalo lingempa fursa ya kuanza kuzungumza na klabu nyingine kuanzia Januari 1 au hata kuingia kwenye mkataba wa awali.
Hata hivyo, United sasa wameamua kurefusha mkataba wake kwa mwaka mmoja.
Chanzo:Bbc
Social Plugin