Mwanamke mmoja Mkazi wa Mburahati NHC, Angelina Joseph (23), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa kosa la kumuua mtoto wake.
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Ramadhan Mkimbo, amedai hayo leo Jumatano Desemba 19, mbele ya Hakimu Frank Moshi.
Amedai Novemba 5 mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa kwa makusudi alisababisha kifo cha mtoto wake mchanga wa siku mbili.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu tuhuma hizo kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kurudishwa rumande hadi Desemba 21, mwaka huu.
Na Aveline Kitomary - Mtanzania