Mbwa Sully akiwa amelala karibu na jeneza lenye mwili wa George HW Bush
Mbwa aliyekuwa amepewa kazi ya kuwa msaidizi wa rais wa zamani wa Marekani George HW Bush amepigwa picha akionekana kuomboleza karibu na jeneza la kiongozi huyo.
Bw Bush, aliyehudumu kama rais wa 41 wa Marekani kati ya mwaka 1989 na 1993 alifariki dunia Ijumaa usiku akiwa na miaka 94.
Sully, mbwa wa jamii ya golden labrador, atasafiri pamoja na mwili wa marehemu kwenye ndege kutoka Texas kwenda DC kwa ndege ya Air Force One - ambayo kwa muda imepewa jina Special Air Mission 41, kwa heshima ya rais huyo.
Mwili huo utarejeshwa Texas Jumatano.
Mbwa huyo wa jina Sully atasindikiza jeneza hilo muda wote.
Chanzo:Bbc
Social Plugin