Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amemtaka mwanachama wa chama hicho, Bernard Membe kufika ofisini kwake ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma za kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli.
Dk Bashiriu alitoa agizo hilo jana Ijumaa akiwa mkoani Geita kwenda kwa mwanadiplomasia huyo aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje utawala uliopita na mgombea urais ndani ya CCM mwaka 2015.
Katibu mkuu huyo amesema Membe anatuhumiwa kuandaa mipango hiyo kimyakimya na tangu ameteuliwa kushika wadhifa huo hajawahi kuonana na Membe
“Kati ya wagombea wote wa CCM ni Membe peke yake ambaye sijakutana naye, namkaribisha ofisini, aje anieleze ninayoyasikia ni kweli au si kweli.”
“Kwani haya yanayozungumzwa nyie hamyasikii? nasema peke yangu? Mimi ndiyo katibu mkuu wa CCM aje ajitetee kwamba yeye si kikwazo,” alisema Dk Bashiru.
“Iweje watu waseme kwamba wewe (Membe) unafanya vikao vya kutafuta kura za 2020, kwamba unataka kumkomesha Rais Magufuli, halafu unakaa kimya tu, sasa mimi nakualika uje ofisini kama ni mwanachama wa kweli aliyetoa ahadi ya uanachama wa CCM ya kusema kweli daima fitina kwangu mwiko njoo ofisini ueleze,” ameongeza.
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA