Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNG'OLEWA MENO YOTE

Mwanamke mlemavu amefariki dunia baada ya meno yake yote kung'olewa katika hatua ambayo imekosolewa vikali nchini Uingereza.

Rachel Johnston alifanyiwa oparesheni hiyo baada ya madaktari kubaini kuwa meno yake yote yameoza.

Lakini alizirai saa kadhaa baada ya kutolewa hospitali ambako alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

Familia yake iliyokuwa imejawa na wasisiwasi ilifahamishwa kuwa madaktari hawakuwa na uwezo wa kuyaokoa maisha yake.

Upasuaji huo ulifanywa na wataalamu wa meno katika kituo cha afya cha Worcestershire.
Familia mbili zaidi zimeiambia BBC masaibu yao kuhusu huduma zinazotolewa na kituo hicho zikisema watoto wao wawili wa kiume walifanyiwa upasuaji bila ya wao kufahamishwa.

Katika visa vyote viwili, familia hizo zilitarajia watoto wao waliyokuwa walemavu watatolewa meno kidogo lakini walistaajabu kuwakuta wakiwa wameng'olewa meno yote.

Rachel Johnston alidungwa sindano ya kufa ganzi katika Kidderminster.

Kituo cha afya cha Worcestershire kinashikilia kuwa kinafuata utaratibu uliyofaa kuwahudumia wagonjwa wake japo kuwa mamlaka kadhaa za matibabu nchini Uingereza sasa zinachunguza kifo cha Johnston.

Makundi ya kutetea haki yanasema kuwa kumekuwa na visa vya mgongano wa mawasiliano kati ya wagonjwa wenye ulemavu na familia zao.

Makundi hayo sasa yanatoa wito kwa madktari wa meno kuingilia kati ili kuzuia visa vya mtu kung'olewa meno yote.

"Haifa kabisa kuona hali kama hii ambapo matibabu yanakuwa ya kushtua," alisema said Sarah Coleman, mkaazi wa Mencap.

Nini kilimfanyikia Rachel Johnston?Diana Johnston anataka kufahamishwa kilichosababisha kifo cha binti yake Rachel

Bi Johnston, 49, amekabiliwa na matatizo ya kuumwa na meno kwa muda hali iliyoifanya familia yake kwenda mbio kumtafutia matibabu.

Mapema mwaka huu familia yake ilifahamishwa kuwa Johnston ''hana budi kung'olewa meno yote''

''Niliuliza kama kuna uwezekano wa binti yangu kung'olwa meno hayo kwa awamu'' anasema mama yake Diana Johnston

Oktoba 26, mwaka huu binti yake ambaye alipata matatizo ya akili baada ya kuugua ugonjwa wa utando wa ubongo akiwa mtoto mdogo alilazwa katika hospitali ya Kidderminster ili kufanyiwa oparesheni ya kung'olewa meno.

''Hali ya bi Johnston haikuwa nzuri wakati wa oparesheni hiyo lakini iliimarika'' alisema mama yake.

Siku iliyofuata, maafisa wa hospitali hiyo walimpigia simu na kumfahamisha kuwa binti yake alikuwa anaumwa.

"Alikuwa anatokwa na damu mdomoni na ulimi wake ulikuwa umefura, huku akiwa amelala kama mtu ambaye hana uhai."

Siku iliyofuata alikimbizwa hospitali baada ya kupatikana na matatizo ya kupumua.

Binti yake alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na baadaye familia ikafahamishwa kuwa madaktari wameshindwa kudhibiti hali yake.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mgonjwa huyo alifariki siku 10 baada ya mashini kuzimwa.

Nini husababisha meno kuoza?
Kuna sababu nyingi zinazofanya meno kuoza ikiwa ni pamoja na kutopiga mswaki, kuongezaka kwa gesi mwilini, na matatizo yanayotokana jeni ya maumbile.

Vituo vya afya ya umma nchini Uingereza hutoa huduma ya kuwaangalia watu waliyo na matatizo ya meno.

Charlotte Waite, mwenyekiti wa chama cha madaktari wa meno nchini Uingereza amesema madaktari lazima wapate idhini ya mgonjwa kumng'oa meno.

"Ikiwa mgonjwa hana uwezo wakutoa idhini , daktari anaruhusiwa kumpatia matibabu kwa kuzingatia maslahi ya afya yake'' alisema Bi Charlotte.

"Sheria inasema daktari amtibu mgonjwa kwa njia ambayo haitaathiri uhuru wake na kumnyima haki zake za kimsingi."

Wataalamu wanasema si rahisi kumfanyia mgonjwa uchunguzi wa meno bila kumdunga sindano ya kufisha ganzi.

Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com