Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MFUNGWA ACHAGUA KUUAWA KWA KITI CHA UMEME

Mfungwa mmoja katika jimbo la Tennessee nchini Marekani atauawa kwa kiti cha umeme baada ya kudai kuwa sindano ya sumu itasababisha ateseke.

David Earl Miller, ambaye amekuwa kwenye hukumu ya kifo kwa miaka 36 ni kati ya wafungwa wanaoongezeka wanaojaribu kukwepa sindano ya sumu kufuatia visa kadhaa vya kufeli.

Mfungwa mwingine huko Tennessee Edmund Zagorski, aliuawa kwa njia ya umeme mwezi uliopita.

Kuuliwa kwa kutumia sindano ya sumu ndiyo njia kuu ya kuwaua wafungwa katika jimbo hilo.

Hata hivyo wafungwa katika jimbo hilo ambao walitenda uhalifu kabla ya mwaka 1999 wataruhusiwa kuchagua kuuliwa kwa njia ya umeme.

Mahakamani, Miller na Zagorski walitaja kisa cha kuuuliwa Billy Ray Irick cha mwezi Agosti ambaye alibadilika rangi kuwa Zambarau na kuchukua dakika 20 kufa.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com