Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MOURINHO 'OUT' MAN UNITED, MRITHI ATANGAZWA


Kocha Jose Mourinho amefutwa kazi na Manchester United ikiwa ni siku moja tu imepita tangu afungwe mabao 3-1 na Liverpool.
Kupitia taarifa yake leo, Man United imeeleza kuwa imefikia uamzi huo ili kunusuru mwenendo wa klabu katika michuano mbalimbali inayoshiriki ikiwemo EPL na klabu bingwa Ulaya.

"Klabu inamshukuru Jose kwa kazi yake nzuri wakati akiwa na Manchester United na tunamtakia mafanikio katika kazi yake hapo baadaye'', imeeleza taarifa ya klabu.

Kiungo wa zamani wa timu hiyo Michael Carrick ametangazwa kuchukua nafasi ya Jose Mourinho kama kocha wa muda wa Manchester United mpaka mwisho wa msimu huu wa 2018/19.

Mourinho alijiunga na Manchester United Juni 2016 akiwa kocha huru baada ya kufukuzwa na Chelsea. Amedumu na Man United kwa takribani miaka miwili na nusu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com