Zikiwa zimebaki siku mbili ili kufanyika kwa kilele cha shindano la urembo la dunia (Miss World), mwakilishi wa Tanzania, Queen Elizabeth Makune, ameendelea kuwa nafasi za juu huku Watanzania wakihimizwa kumpigia kura kwa wingi ili ashinde.
Queen Elizabeth ambaye yupo Sanya China tayari kwa mashindano hayo yanayojumuisha warembo zaidi ya 50 kutoka nchi mbalimbali duniani, amesema bado anahitaji kura ili aweze kutwaa taji hilo.
“Naomba Watanzania wenzangu pamoja na wadau wa urembo wanipigie kura ili niweze kuingia katika nafasi ya ushindi ili kupeperusha vyema bendera yetu, mpaka sasa nipo katika nafasi nzuri,” alisema Queen.
Social Plugin