Diwani wa zamani wa kata ya Nyerere, Unguja Asha Ali Abei amejinyonga hadi kufa usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 26, 2018.
Akizungumza leo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, Kheri Musa amesema marehemu ambaye kwa miaka ya nyuma alikuwa diwani, alikutwa amekufa kwa kujinyonga akitumia mtandio alioufunga katika dirisha, tukio lililotokea katika shehia ya Magomeni.
Baadhi ya majirani wa marehemu walisema kwamba walipata taarifa za kifo hicho asubuhi baada ya mtoto wa marehemu kupiga kelele.
Sheha wa shehia ya Magomeni, Rajab Ali Ngauchwa amesema si vyema wananchi kuchukua hatua za haraka katika mambo yanayowachanganya.
Amesena ni vyema familia kukutana na kujadili ili kupata ufumbuzi wa tatizo kuliko watu kuchukua uamuzi kama huo wa kujitoa uhai.
Social Plugin