Binti wa miaka mitatu yupo mahututi hospitalini nchini India baada ya kubakwa Jumapili Desemba 16.
Mtuhumiwa, mwenye umri wa miaka 40 ni mlinzi katika jengo ambalo mtoto huyo anaishi, na tayari ameshakamatwa.
Polisi walimkuta mtoto huyo akiwa amepoteza fahamu na kumkimbiza hospitali ambapo anafanyiwa upasuaji.
Tukio hilo limetokea jana ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya miaka 6 tangu kubakwa kwa mwanafunzi na genge la wahuni katika basi jijini Delhi.
Kamishina wa masuala ya wanawake huko Delhi Swati Maliwal amesema tukio hilo limeangusha kumbukumbu ya mwathirika wa ubakaji katika basi ambapo tukio hilo lilipelekea kuibuka kwa maandamano makubwa nchi nzima na kuongeza makali katika sheria ya ubakaji.
Chanzo:Bbc
Social Plugin