Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha :MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI (MUHAS) YAFANA JIJINI DAR

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, Profesa Andrea Pembe. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akiwakaribisha wakufunzi kusoma majina ya wahitimu.
Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamili, mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahitimu waliotunukiwa astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es salaam.
Bendi ya Jeshi ikisherehesha katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimtunuku astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika jijini Dar es salaam. 
Wahitimu wa astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili katika upande wa afya wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakila kiapo cha uaminifu wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Wahitimu wakifurahia.
Meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa kuhitimisha sherehe.
Meza kuu ikipata picha na baadhi ya wahitimu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com