Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MVUA YAUA WAWILI KANISANI KAHAMA, 10 WAJERUHIWA


 Watu wawili wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa baada ya ukuta wa ndani ya kanisa la SDA Wasabato lililopo Igomelo Mjini Kahama mkoani Shinyanga kuanguka kutokana na mvua iliyoambata na upepo mkali kunyesha.


Kwa Mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule tukio hilo limetokea Disemba 16,2018 majira ya saa 10 na nusu jioni.

Aliwataja waliofariki kuwa ni Juneth Edward Ngusa (35) na Elisha Masai (05) wote wakazi wa Igomelo.

Waliojeruhiwa ni  Eva Simon (30),Upendo Daniel (25),Ayubu Kisunda (37),Mary Maduhu (35),Stephen Shija (23),Paulo Ibrahim (25), Jacklin John (25), Irene Daniel (05), Rahel Emanuel (30) na Marium Kishegena (30).

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com