MWAKYEMBE APELEKA KWENYE VYOMBO VYA USALAMA MAJINA YA WANACHAMA WA YANGA

Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwanyembe amepeleka majina nane ya wanachama wa klabu ya Yanga kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya kuwachunguza.
 
Akisoma taarifa ya Waziri Mwakyembe kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Ufundi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Yusuph Singo amesema Mh. Mwakyembe hafurahishwi na vitendo vya wanachama hao.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa wanachama hao wanaoongozwa na Bakili Makele, wanahamasisha wanachama wengine kupinga uchaguzi wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 13, 2019.

Taarifa hiyo imesema kuwa wanachama hao wakiongozwa na Bakili wanahamasisha wanachama kususia uchaguzi wakishinikiza kuwa Mwenyekiti wao Yusuph Manji bado yupo madarakani.

Wanachama hao ni:-
  1. Bakili Makele
  2. Mustaph Mohammed
  3. Said Bakari
  4. Shaban Mgonja
  5. Kitwana Kondo
  6. Boaz Kupilika
  7. David Sanare
  8. Edwin Kaisi.
Bakili ambaye alikuwa Mwenyekiti wa matawi ya Yanga huku Boaz akiwa Katibu wake walifungiwa kujihusisha na soka miaka mitano na faini ya milioni mbili na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa kosa hilo hilo wiki kadhaa zilizopita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم