Mbunge wa Mtama na Waziri wa zamani wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameshindwa kuficha hisia zake juu ya ushindi walioupata timu ya Simba dhidi ya klabu ya Nkana ya Zambia.
Nkana ambayo ilichuana na Simba leo Jijini Dar es salaam kwenye Uwanja wa Taifa ilishuhudia Simba ikifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano klabu bingwa Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1.
Kupitia ukurasa wake Twitter Nape Nnauye ameandika ameshindwa kujiuzuia moja ya goli lilifungwa na mshambuliaji Clatous Chama na kusema bao hilo ni la aina yake.
"Nimejificha vya kutosha, lakini kwa goli hili, Simba hii kiboko This is Simba" aliandika Nape.
Watu wengine mashuhuri wakiwemo mastaa wa filamu na muziki wameelezea furaha zao juu ya ushindi wa Simba kama inavyoonekana hapo chini.
Social Plugin