Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 30, anapigiwa upatu kuhamia klabu ya Inter Milan msimu huu wa joto.
Ozil, ambaye aliachwa nje ya kikosi kilichocheza dhidi ya Bournemouth wiki iliyopita alikosa derby ya London kaskazini kutokana na maumivu ya misuli, ilisema Arsenal.
Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri ya kwamba hakuwa na uhakika ikiwa Ozil angelihudhuria mechi ya Arsenal dhidi yaTottenham ambapo waliibuka kidedea.
Aston Villa imefanya mazungumza na Chelsea kuhusiana na uhamisho wa Tammy Abraham kwa mkopo - wana matumaini makubaliano hayo ya msimu mzima na shambuliaji huyo wa miaka 21 hayatatibuka.
Chanzo:Bbc
Social Plugin