Pambano hilo lililofanyika nchini Marekani lilionekana kuwa upande wa Fury ambaye alirejea katika ulingo baada ya kutoonekana kwa muda wa miaka miwili na nusu.
Wilder alichochea konde la kushoto na kumuangusha mpinzani wake mara mbili kwenye sakafu katika raundi ya tisa, na akidhani alikuwa amekamilisha kazi, kabla ya Fury kuamka na kumshangaza Wilder kwa mapigo ya kasi na yenye nguvu yaliyomshinda hadi raundi ya mwisho.
Akiongea baada ya pambano hilo, Fury amesema, " Niliangushwa chini mara mbili lakini nilikuwa bado nina nguvu na ninaamini kwamba nimeshinda pambano hili, nitaendelea kubakia na kiwango changu, nilikwenda Ujerumani nikamchapa Klitschko na nimekuja hapa najiona kama nimemshinda Wilder".
Mabondia hao wawili wanaendeleza rekodi yao ya kutopoteza pambano ambapo sasa, Fury ameshuka ulingoni mara 28 na kushinda 27, mara 19 kati ya mapambano aliyoshinda ikiwa ni kwa KO huku akitoka sare pambano moja. Wilder yeye ameshuka dimbani mara 41 na kushinda 40 mapambano 39 akishinda kwa KO na kutoka sare pambano moja.
Chanzo:Eatv