Wakazi katika jiji la kusini-mashariki mwa nchi ya China mwishoni mwa juma lililopita walifanikiwa kumpata mshindi wa shindano la aina yake la kula pilipili.
Mwanadada, Yi Huan aliibuka kidedea kwenye mashindano hayo na kuvishwa taji la ‘Chilli Queen’ baada ya kula pilipili 20 chini ya dakika moja.
Shindano hilo lililofanyika siku ya Jumapili katika jimbo la Jiangxi, limeshuhudiwa washiriki wengi wakiwemo wanaume kushindwa kufuadafu mbele ya Yi Huan.
Picha nyingine zinazowaonyesha washiriki hao wakishindana kula pilipili.
Social Plugin