Mwanamume aliyeuawa kimakosa jimboni Alabama, Marekani ameuawa kwa kupigwa risasi mara tatu kutoka nyuma, uchunguzi wa maiti yake umebaini.
Emantic Bradford Jr, anayefahamika kama EJ, alipigwa risasi kichwani, shingoni, na kwenye mfupa wa nyonga akiwa katika jumba la kibiashara la Riverchase Galleria mjini Hoover, Alabama.
Polisi walikuwa wamedhania yeye ndiye mshambuliaji aliyewaua watu wawili kwa kuwapiga risasi - mwanamume mmoja wa miaka 18 na msichana wa miaka 12 mwezi jana.
Lakini baadaye polisi walikisi kwamba walikuwa wamekosea, na sasa wamemkamata mwanamume mwingine wanayesema ndiye mshukiwa halisi.
Mwanamume huyo anayezuiliwa kwa sasa, Erron Brown, 20, alijisalimisha mwenyewe kwa polisi.
Chanzo:Bbc
Social Plugin