Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA BAADA YA KUUA WANAWAKE 77


Polisi mmoja wa zamani nchini Urusi ambaye anatajwa kama muuwaji wa watu wengi zaidi kwa miaka ya hivi karibuni nchini humo amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mara ya pili.

Mikhail Popkov, mwenye miaka 53, amekutwa na hatia ya kuuwa wanawake 55 na polisi mmoja mwanaume kati ya mwaka 1992 na 2007.

Popkov tayari anatumikia kifungo cha awali cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kuuwa wanawake 22 hapo awali.

Aliwauwa wanawake wote hao baada ya kuwapatia usaidizi wa kuwapakia katika gari yake usiku wa manane. Kati yao 10 aliwabaka.

Popkov alitiwa nguvuni mwaka 2012 baada ya uchunguzi wa vinasaba yaani DNA kushabihiana na gari lake.

Wanawake hao walikuwa kati ya miaka 16 na 40, katika matukio hayo ya mauaji takriban mara tatu alitumia gari ya doria ya polisi.

Mauaji hayo yametekelezwa katika jiji la Angarsk kwa kutumia shoka na nyundo. Popkov alitupa mabaki ya miili ya wanawake hao baada ya kuikatakata kwenye mapori, kando ya barabara ama makaburini.

Popkov amedai alikuwa "akilisafisha" jiji la Angark na wanawake wasiokuwa na maadili.

Popkov ametekeleza mauaji zaidi ya Alexander Pichushkin aliyeua watu 48, na Andrei Chikatilo aliyeua watu 52 wote wakati wa zama za Urusi ya Kisovieti.Haki miliki ya pichaAFPImage captionPopkov akiwa mahakamani: aliacha kazi ya polisi mwaka 1998

Alama za matairi ya gari ya Niva iliyokuwa ikimilikiwa na Popkov iligunduliwa pembeni ya baadhi ya miili ya watu aliowaua. Hali hiyo iliwalazimu polisi kuchunguza wamiliki wote wa magari ya aina ya Niva kwenye jiji la Angarsk.

Uchunguzi wa vinasaba vya DNA viliwafikisha polisi mpaka kwenye gari la Popkov na baada ya kushabihiana alitiwa nguvuni.

Alikamatwa akiwa njiani kuelekea jiji la Vladivostok kwa malengo ya kuknunua gari jipya. Baadae alikiri kuuwa wanawake 20. Mhanga wake mdogo zaidi ni binti wa miaka 15 aliyekuwa bado ni mwanafunzi wa sekondari.

Mahakama jijini Irkutsk ilimkuta na hatia ya kuua wanawake 22 mnamo mwaka 2015 na kumpa kifungo cha maisha jela. Hata hivyo aliendelea kushikiliwa rumande baada ya uchunguzi mpya wa mauaji zaidi kufunguliwa.

Shirika la habari la Interfax limeripoti kuwa Popkov alijigamba mbele ya mfungwa mwenzake kuwa ameuwa watu wengi kuliko Chikatilo.

Uchunguzi wa kitabibu ulionesha kuwa Popkov ana akili timamu lakini aligunduliwa pia kuvutiwa na kuuwa watu, kwa mujibu wa waendesha mashtaka.

Baadhi ya wale aliowashambulia walipatikana bado wangali hai lakini walifariki baada kufikishwa hospitali.

Mwendesha mashtaka Alexander Shkinev amesema Popkov anatarajiwa kukata rufaa ili aendelee kulipwa pensheni yake ya polisi ya rouble 24,000 rkwa mwezi sawa na 361 kwa hoja ya kuwa alitoa ushirikiano kwa wapelelezi.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com