Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Video:MEYA ARUHUSU POLISI WA KIKE KUVAA KAPTULA FUPI KAMA SARE ZA KAZI

Kutana na hii kutokea nchini Lebanon ambapo polisi wa kike wameruhusiwa kuvaa kaptula wakiwa kazini wakati wakiongoza magari barabarani hii ni baada ya Meya wa mji wa Broummana Pierre Achkar kutangaza kaptula kuwa uniforn wakati wa majira ya joto.

Pierre Achkar amesema kuwa kila mwaka anajaribu kufanya kitu cha tofauti ili kuvutia vyombo vya habari vya kimataifa ikiwa na kuwavutia watalii wanaoingia katika mji huo wa Broumanna huku akiamini kila kitu kinabadilika duniani kulingana na wakati.

Baadhi ya wananchi wa Lebanon wameonekana kukubaliana na maaumizi hayo mapya yaliyofanya na Meya huyo huku wengine wakimkosoa wakisema anatumia warembo hawa kuvutia watalii.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com