Jengo lililofungwa rada mpya kwa ajili ya kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
***
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mfumo wa rada ya kuongozea ndege nchini unaojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza na wanahabari waliofanya ziara ya kutembelea ujenzi huo, Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa amesema ujenzi wa jengo hilo umekamilika na ufungaji wa vifaa unaendelea hivyo ifikapo Desema 21 wataweza kufanya majaribio.
"Kama mnavyoona wanahabari kila kitu kimeshafanyika tunachomalizia ni mitambo midogo midogo inayotarajia kukamilika ifikapo wiki ijayo na tufanye majaribio ili kuona ni wapi pa kurekebisha au tuongeze kitu gani?," amesema Mwakisasa.
Nae mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye amesema mara baada ya kukamilika na kuanza kufanya kazi, mfumo huo utaimarisha zaidi ulinzi wa anga la Tanzania.
Amesema kwa kiasi kikubwa rada hiyo pamoja na zile zitakazojengwa Mwanza, Songwe na Kilimanjaro zitasimamiwa na TCAA ikiwamo kuziongoza ili kuhakikisha ulinzi unaimarishwa zaidi.
Jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo huo wa rada liliwekwa Aprili 2, 2018 na Rais John Magufuli na utagharimu Sh67 bilioni zikijumuisha mfumo wa rada uliojengwa katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.
Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa akitoa ufafanuzi juu ya masuala yanayohusu ujenzi huo.
Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa akitoa ufafanuzi juu ya masuala yanayohusu ujenzi huo.
Mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye akieleza machache juu ya ujenzi huo wa rada mpya.
Wanahabari waliofanya ziara katika mnara wa kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya akina mama muongoza ndege Bi. Mossy Kitang'ita akiwajibika.
Wanahabari wa vyombo mbali mbali wakipata maelezo kuhusu masuala yahusuyo usafiri wa anga.
Social Plugin