Shirika lisilo la serikali la Rafiki Social Development linalojihusisha na kutetea haki za binadamu na usawa katika jamii,limeendesha midahalo ya kuzihamasisha jamii kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kutoa elimu inayolenga mabadiliko ya kitabia.
Midahalo hiyo imefanyika katika kata ya Lyabukande,Iselamagazi,Mwakitolyo na Salawe ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia,zikiwemo ndoa na mimba za utotoni.
Wakazi wa maeneo hayo wamesema vitendo vya ukatili wa kijinsia vimezidi kushamiri kwasababu ya baadhi ya mila na desturi kandamizi,mfumo dume ,umasikini na kukosa elimu ya haki za binadamu.
Aidha waliongeza kuwa wamekuwa wakikabiliwa vitisho vya ushirikina na vipigo pindi wanapojitokeza kutoa taarifa kwenye mamlaka,kwani baadhi ya watendaji wamekuwa wakivujisha siri kwa mtuhumiwa hali inayoleta uadui kati yao.
Afisa maendeleo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Opeyo Sisso amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya ukatili vinapotokea kwenye maeneo yao,kuacha uoga wa kutoa taarifa hizo ni kuendeleza ukandamizwaji hasa kwa wanawake na watoto.
“Jamii muache uoga wa kutoa taarifa pindi unapoona viashiria vya ukatili kwa viongozi wa serikali ili kuvizuia visitokee na kuleta madhara,mbona mnapoibiana hamuogopi kutoa taarifa,jamani tubadilike tuunge mkono juhudi hizi.” Alisema Sisso
Lengo la midahalo hilo ambayo imeambatana na uonyeshaji sinema ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu mfumo sahihi wa utoaji wa taarifa za ukatili wa kijinsia lakini pia kuzifahamu haki za binadamu na usawa.
Picha zote na Malaki Philipo
Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Opeyo Sisso akiwahimiza wananchi kutoa ushirikiano katika vita dhidi ya vitendo vya ukatili.
Wajumbe wa mdahalo Kata ya Lyabukande wakifuatilia hoja zinazo wasilishwa katika mjadala wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Viongozi wa serikali ngazi ya kata wakiandika dodoso (kushoto mwanzo )Harun Ibrahim Afisa mtendaji wa kata ya Lyabukande(kulia mwanzo) Salum Mwang'imba afisa maendeleo ya jamii kata ya Lyabukande.
Mwalimu Upendo Dickson akichangia kuwahusisha wazazi na uwepo wa matukio hayo kwasababu wamekuwa hawatoi ushirikiano tatizo linapotokea.
Mwanasheria Senorina Kisunzu akitoa ufafanuzi wa sehemu sahihi za kutoa taarifa za ukatili ambazo ni kuanzia uongozi wa serikali ngazi ya kitongoji.
Wazee maarufu pamoja na viongozi wa dini kata ya Iselamagazi wakifuatilia mdahalo.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mtoto kata ya Iselamagazi wakichangia nafasi ya vijana kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Mdahalo ukiendelea wajumbe wa kata ya Iselamagazi eneo ambalo baadhi ya wananchi wamesema wanakabiliwa n tishio la kurogwa na vipigo wanapotoa taarifa za ukatili
Social Plugin