ROBOTI YAGEUKA MTU..GUMZO KILA KONA


"Roboti" mtu au mtu Roboti!

Roboti moja iliyokuwa kwenye tamasha la maonesho yaliyofadhiliwa na taifa ilishangaza wengi kwa uwezo wake wa juu.

Roboti Boris aliyeonyeshwa katika kipindi cha runinga nchini humo, alionesha uwezo mkubwa wa kutembea, kuongea na kucheza dansi.

Lakini muda mfupi baadaye, waandishi habari wakahoji uwezo mkubwa wa roboti hiyo.

Katika picha ambayo ilichapishwa baadaye kwenye mitandao ya kijamii, shingo ya binadamu, ilionekana bayana.

Loh, ukweli ukabainika kuwa halikuwa roboti bali mtu aliyevalia magwanda ya plastiki tu.

Vazi hilo liitwalo Alyosha the Robot, lililoundwa na kampuni iitwayo Show Robots na linagharimu dola 2,975.uku waandalizi wa tamasha la teknolojia ya Proyektoria - wakiwalenga vijana chipukizi katika maonyesha hayo, wakiwa bado hawajatangaza kuwa kwa hakika hilo lilikuwa Roboti- matangazo ya runinga ya Russia-24, yalitangaza kuwa ni roboti halisi.

Tovuti ya mtandao wa TJournal nchini Urusi, ndio iliyokuwa ya kwanza kushuku iwapo hiyo ilikuwa ni roboti halisi au la....ikiuliza maswali chungu nzima ikiwemo:
  • Ni kwa nini muundo wa roboti hiyo haina vifaa vya kutuma na kupokea ujumbe maarufu kama sensors?
  • Jinsi gani wanasayansi wa Urusi walifaulu kuunda roboti haraka hivyo, huku kukiwa hakuna taarifa au ripoti zozote zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari kuhusiana na maandalizi ya uundaji.
  • Je, mbona hakuna taarifa zozote za utalamu huo wa kisasa kwenye mitandao ya kijamii?
  • Mbona roboti ilikuwa ikifanya ishara nyingi pale lipokuwa ikicheza muziki?
  • Kwanini ilikuwa na umbo ambalo binadamu anaweza kuingia ndani na kutoshea barabara?
  • Kwanini sauti yake ilikuwa imerekodiwa badala ya kutoa sauti moja kwa moja mbele ya umati?
Katika tovuti ya kampuni hiyo iliyounda vazi hilo la Alyosha Robot, bidhaa hiyo inaelezewa kama iliyo na uwezo "sawa kabisa na roboti halisi".
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
أحدث أقدم