Kocha wa klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri ameelezea kile alichokitarajia wakati Cristiano Ronaldo alipoteuliwa kuchukua nafasi ya kuwa mpiga penalti wa klabu hiyo.
Massimiliano Allegri amesema kuwa amemuamini Ronaldo kuwa mpigaji wa penalti tangu mchezaji huyo alipopiga penalti na kuifungia Real Madrid katika mchezo dhidi ya Juventus dakika ya 93 katika mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya msimu uliopita.
Mkwaju wa penalti wa Cristiano Ronaldo dakika ya 93 ndio ulioiondoa Juventus katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mwezi April mwaka huu.
Alipoulizwa kuhusu Ronaldo kuchukua nafasi ya kuwa mpigaji wa penalti katika klabu yake, Allegri amesema kuwa hiyo ni moja ya njia ya kuwafanya mashabiki wamsamehe kutokana na ushujaa wake dhidi ya Juve katika michuano ya klabu bingwa.
"Baada ya kutufunga bao lile dhidi yetu katika dakika ya 93 ya mchezo, nina haja ya kumchagua mtu mwingine kufanya hivyo?, anatakiwa afanye hivyo ili asamehewe. Anatakiwa awe anapiga penalti na kufunga mara kwa mara," amesema Allegri.
Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza wa Juventus tangu John Charles (1957-58) kufunga mabao 10 au zaidi katika mechi 14 za msimu wake wa wa kwanza wa Serie A.
Nyota huyo wa Kireno , amefunga mabao 11 katika michezo 18 aliyoichezea Juventus msimu huu. Juve inaongoza kwa tofauti ya pointi 11 katika msimamo wa Serie A , baada ya kushinda michezo yake 13.
Social Plugin