Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) imeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuongeza jitihada zaidi za kuwajengea uwezo
wanafunzi na wahadhiri juu ya masuala ya rushwa hasa ya ngono kwa lengo la kupunguza au kumaliza kabisa tatizo hilo vyuoni.
TSNP umesema kuwa rushwa ya ngono kwa sasa imeshamiri katika vyuo mbalimbali nchini hivyo inapaswa kukemea kwani inaharibu maisha ya wanafunzi ambao wanategemewa kuwa viongozi wa baadae.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu wa TSNP, Joseph Marekela alisema rushwa ya ngono vyuoni ni changamoto kubwa hasa kwa wanafunzi wa kike hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kuhakikisha kuwa
hakuna mtu anayepoteza haki yake ya msingi kwa kukataa kutoa rushwa hiyo ambayo si tu inapoteza utu wa mtu bali ni kinyume na haki za binadamu.
Alisema mfumo wa upimaji uwezo uliyopo sasa umempa mamlaka makubwa mhadhiri ya kuamua hatma ya mwanafunzi kitaaluma jambo ambalo lina
sababisha uwepo wa mianya ya rushwa ya ngono kwa wahadhiri wasio na maadili ambao wanatumia nafasi yao kuminya haki ya mwanafunzi.
“Kwakuwa tatizo hili ni kubwa na limeathiri wanafunzi wengi chuoni tunatoa wito kwa Takukuru waongoze jitihada zaidi kwa kuwajengea uwezo taasisi za
Takukuru vyuoni ili kupambana na tatizo hili kikamilifu, pia vituo vya jinsia na Serikali za wanafunzi ziwajibike ipasavyo ili kuhakikisha kuwa hakuna anaepoteza haki yake ya msingi kwa kukataa kutoa rushwa hiyo ya ngono,” alisema.
Hata hivyo mtandao huo umesema kuwa ukosefu wa taulo za kujisitiri wanafunzi wa kike hasa wa vijijini kipindi cha hedhi inaathiri maendeleo ya wanafunzi
hao kitaaluma.
Kutokana na hali hiyo, Marekela alisema wanatoa wito kwa Serikali kupitiaWizara yenye dhamana kulitazama upya suala kwa kugawa bure taulo hizo kwa
wanafunzi wa kike hasa waliopo maeneo ya vijijini ili kunusuru ndoto zao walizojiwekea.
Aidha alisema suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu bado ni changamoto kwani wengi wao wameshindwa kuendelea na masomo kwa kukosa mikopo hiyo
Social Plugin