LEMA ATUMA OMBI KWA RAISI MAGUFULI

Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuzungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga kwa kile alichodai kuwa ametoa kauli tata.

Lema kupitia ukurasa wake wa kijamii leo, Disemba 16, ameandika kuwa kauli ya Gavana ambayo hakuianisha ni kauli ipi, kuwa endapo isipoeleweka hata kama iliongelewa kwa nia njema itakuwa ni hatari kwa mstakabali wa uchumi.

"Mh Rais tafadhali kwa heshima kabisa ongea na Gavana wa Benki kuu ,kwa maoni yangu Gavana anaongea sana.Kauli ya Gavana hata kama ina nia njema ikishindwa kueleweka mara nyingi huwa ni hatari kwa uchumi na uimara wa shilingi. Sina uhakika kama utadumu naye muda mrefu kazini", ameandika Lema.
Mh Rais tafadhali kwa heshima kabisa ongea na Gavana wa Benki kuu ,kwa maoni yangu Gavana anaongea sana.Kauli ya Gavana hata kama ina nia njema ikishindwa kueleweka mara nyingi huwa ni hatari kwa uchumi na uimara wa shilingi. Sina uhakika kama utadumu naye muda mrefu kazini.
44 people are talking about this

Mh Rais tafadhali kwa heshima kabisa ongea na Gavana wa Benki kuu ,kwa maoni yangu Gavana anaongea sana.Kauli ya Gavana hata kama ina nia njema ikishindwa kueleweka mara nyingi huwa ni hatari kwa uchumi na uimara wa shilingi. Sina uhakika kama utadumu naye muda mrefu kazini.

Novemba 20, katika mkutano wake na wanahabari, Prof. Luoga alisema kuwa taasisi hiyo imeanzisha operesheni maalum ya ukaguzi na udhibiti wa uendeshaji biashara ya fedha jijini Arusha, ikiwa ni siku moja tangu kutokea sintofahamu katika biashara ya maduka ya kubadilishia fedha jijini humo baada ya kufungwa kwa saa kadhaa.

“Uchunguzi wa Benki Kuu umebaini kuongezeka biashara ya ubadilishaji na utakatishaji fedha. Kuna maduka hayajasajiliwa lakini yanafanya biashara hii kinyume cha utaratibu,” alisema Profesa Luoga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post