Klabu ya soka Simba imefanikiwa kuingia hatua ya kwanza ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 ugenini dhidi ya Mbabane Swallows na kuvuka kwa jumla ya mabao 8-1.
Mabao ya Simba katika mchezo wa leo yamefungwa na kiungo Clatous Chama ambaye amefunga mabao mawili katika dakika za 28 na 32. Mabao hayo yalidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili washambuliaji Emmanuel Okwi na Meddie Kagere walifunga bao moja kila mmoja, hivyo kufanya mchezo umalizike wakiwa wanaongoza kwa mabao 4-0. Ushindi wa jumla sasa umekuwa ni 8-1 baada ya wiki iliyopita kushinda kwa mabao 4-1 jijini Dar es salaam.
Kwa upande wa wawakilishi wengine wa Tanzania klabu ya Mtibwa Sugar inayocheza kombe la shirikisho imeshinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Haruna Chanongo na kufikisha mabao 5-0 baada ya kushinda 4-0 jijini Dar es salaam.
Simba na Mtibwa sasa zitasubiri droo ichezeshwe na shirikisho la soka barani Afrika (CAF), ili kujua watakutana na timu gani katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo.
Social Plugin