Klabu ya soka ya Simba imeng'olewa katika michuano ya shirikisho (Azam Sports Federation Cup) baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Mashujaa FC .
Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa taifa, Simba imefungwa mabao 3-2 na kuwaondoa kabisa katika mshindano hayo.
Mabao ya Mashujaa FC yamefungwa na Shaaban Hamis katika dakika ya 47, Jaremiah Josephat katika dakika ya 57 na Rajabu Athuman huku mabao ya Simba yakifungwa na Paul Bukaba katika dakika ya 19 na 79.
Simba imeondolewa katika michuano hiyo kwa msimu wa pili mfululizo, ambapo msimu uliopita iliondolea katika hatua hii kwa kufungwa na Green Warriors kwa mikwaju ya penati 4-3.
Inabakiza nafasi mbili pekee za kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, ambazo ni Ligi Kuu Tanzania Bara endapo itaibuka bingwa pamoja na michuano ya Klabu Bingwa Afrika endapo itashinda ubingwa huo.
Matokeo ya mchezo mwingine ni ya Mtibwa Sugar na Kiluvya United, ambapo Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kuungana na vigogo wengine wakiwemo Yanga na Azam FC ambao wanafuzu hatua inayofuata ya 32 bora.
Social Plugin