Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TETESI ZA SOKA LEO BARANI ULAYA CHELSEA KUMSAJILI PULISIC

Chelsea kwa mara ya kwanza imewasiliana rasmi na Borussia Dortmund kuhusu nia yao ya kutaka kumsajili winga wa Marekani Christian Pulisic, lakini huenda klabu hiyo ya Ujerumai ikaitisha euro milioni 70 ili kumuachia mchezaji huyo mwenye miaka 20 ambaye anapania kujiunga na klabu ya Liverpool. 


Kiungo wa kati wa Uhispania Brahim Diaz, 19, anajiandaa kuondoka Manchester City na kujiunga na Real Madrid, licha ya ombi la Pep Guardiola la kumtaka asalie katika klabu hiyot. 

Meneja wa Arsenal Unai Emery anasema kuimarika kwa kiwango cha Aaron Ramsey ni jambo jema kwa kiungo huyo wa Wales wa na kwamba uamuzi wa klabu hiyo ni kutoweka wazi kandarasi yake. 

Vilabu vya Crystal Palace, Bournemouth, West Ham, Newcastle vinavyoshiriki ligi ya primia pamoja na Schalke ya Ujerumani vinapania kumsajili kiungo wa kimataifa Ruben Loftus-Cheek, 22, anayechezea klabu ya Chelsea baada ya kiungo huyo kukiri kuwa hali ni ''ngumu'' kutokana na kutopangwa katika kikosi cha kwanza.

Mshambuliaji wa West Ham na Mexico Javier Hernandez, 30, ana mpango wa kuhama klabu hiyo mwezi ujao.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com