Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa amedai kuwa kwa sasa jamii imekosa hali ya upendo hali inayosababisha kuongezeka kwa matukio ya mahusiano mengi kuvunjika.
Askofu Malasusa amesema kauli hiyo Desemba 25, 2018 katika ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam ambapo amesema wana ndoa wengi wanahofu na mahusiano.
“Siku hizi talaka zimezidi jamii haina upendo wala hofu ya Mungu, hofu imejaa katika ulimwengu, wengi waliopo katika ndoa hawana hakika kama wataendelea,’’ amesema.
Aidha ameongeza kuwa “malaika anasema usiogope nitawaletea habari njema, tena katika aya yetu ya siku ya leo tunasema tumepewa mtoto mwanamume, yeye yupo tayari kubadilisha mitazamo yetu kutuondoa katika hofu na kuwa wajasiri katika maisha yetu.”
Mamilioni ya waumini wa dini ya kikristo Duniani leo Desemba 25 wanaadhimisha sikukuu ya Krismasi ikiwa kukumbuka ya siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Social Plugin