Kampuni ya TBL Group, imeadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani kwa wafanyakazi wake kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Moshi na Arusha, kushiriki zoezi la upimaji wa afya zao,kufanya mazoezi na kutoa misaada kwa vituo vinavyolea watoto yatima.
Afisa Mahusiano ya wafanyakazi wa TBL Group,Salma Nyangasa,alisema maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yamekuwa yakiadhimishwa na kampuni kila mwaka kwa kuwashirikisha wafanyakazi wake kupima afya zao.
“Suala la afya za wafanyakazi ni jambo ambalo kampuni inalipa umuhimu mkubwa ndio maana tumetumia siku hii kupima afya sambamba na kushiriki kufanya mazoezi ya kujenga mwili na kupatiwa semina za kukabiliana na magonjwa mbalimbali”alisisitiza.
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Ilala wakishiriki zoezi la kupima afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiwasha mshumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakishiriki mazoezi wakati wa siku ya kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha TEHAMA (IT) wa TBL, wakikabidhi msaada kwa Mkuu wa kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Msimbazi Centre,Sister Stela, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
Social Plugin