AC Milan imemweka mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa Uingereza Marcus Rashford, 21, katika orodha ya wachezaji inayopania kuwanunua wakati dirisha la usajili litakapo funguliwa mwezi Januari.
Hii ni baada ya juhudi zao za kumnunua nyota wa Uswidi, Zlatan Ibrahimovic kugonga mwamba. (Gazzetta dello Sport)
Beki wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Belgium Vincent Kompany, 32, anapigiwa upatu kujiunga na Barcelona. (Sun)
Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, 25, ameshangazwa na hatua ya meneja wake Jose Mourinho, kumuacha nje ya kikosi cha kwanza cha klabu hiyo katika mechi mbili zilizopita. (Guardian)
Chelsea inampango wa kumsaini beki wa kulia wa Napoli Elseid Hysaj, 24. (Calciomercato)
Manchester United nayo inamlenga mlinzi wa kati wa Bordeaux, Mbrazil Pablo, 27. (Fox Sports)
Tetesi zimeibuka kuwa kingo wa Real Valladolid inayoshiriki ligi ya Uhispania, Fernando Calero, 23, analengwa na Arsenal. (Team Talk)
Newcastle wako tayari kumuachilia kiungo wa kati wa Benfica, Andreas Samaris wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugiriki amekuwa akilengwa na vilabu kadhaa. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Manchester United na timu ya taifa ya Uhispania Juan Mata, 30, amesema kuwa"anafurahia sana" uwepo wake Old Trafford huku mazungumzo kuhusiana na kurefushwa kwa kandarasi yake katika klabu hiyo ikiendelea. (Manchester Evening News)Juan Mata, kiungo wa kati wa Manchester United
Tottenham wameonesha nia ya kumsajili nyota wa Uhispania Marco Asensio, 22 anayechezea Real Madrid. (Marca - via Mirror)
Liverpool inapania kumnunua kiungo wa kati wa Brighton na timu ya taifa ya Ujerumani Pascal Gross, 27, mwezi Januari huku meneja wake Jurgen Klopp akipendekeza kuwenka dau la euro milioni 15m. (Mirror)
Chelsea wanatafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona ambaye pia aliwahi kuichezea Manchester City Denis Suarez, 24, wanapojiandaa kumuachilia Cesc Fabregas. (Mirror)
Leicester City hawana mpango wa kumsajili mchezaji yeyote mpya mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa, kwasababu meneja wake Claude Puel ameridhika na kikosi kilichopo sasa. (Leicester Mercury)
Meneja wa Shanghai SIPG, ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuchukuwa usukani katika klabu ya Reading. (Sky Sports)
LA Galaxy inajiandaa kumsajili tena mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 37, kwa mkataba mpya, kufuatia tetesi kwamba huenda akarejea AC Milan. (ESPN)Zlatan Ibrahimovic, mshambuliaji wa Uswidi
Winga wa zamani wa Ufaransa Franck Ribery, 35,anajiandaa kuondoka Bayern Munich mwisho wa msimu huu, hayo ni mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Ujerumani Hasan Salihamidzic. (Bild - kwa Kijerumani)
Manchester United wanammezea mate winga wa Middlesbrough, Muingereza Marcus Tavernier, 19. (Mail)
Juhudi za klabu ya Galatasaray kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Ubelgiji Divock Origi zimegonga mwamba baada ya klabu yake kusisitiza kuwa inaMtaka kiungo huyo wa miaka 23 kuishi karibu na Uingereza.
Barcelona haitamruhusu mshambuliaji wake Ousmane Dembele, 21, kuhama klabu hiyo bila ya kulipwa chini ya euro milioni 400 ambacho ni kifungu cha kumuondoa katika mkataba. (Mundo Deportivo)(ESPN)Ousmane Dembele mshambuliaji wa Barcelona
Tetesi bora ya Jumanne
Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 27, amezungumzia tena kuhama kwenda Real Madrid na anasema kuwa hajui ni lini ataamua hatma yake.
Lakini Mbelgiji huyo amekiri kuwa mazungumzo kuhusu mkataba mpya huko Stamford Bridge yamekwama. (RMC Sport via Express)
Mkurugenbzi wa michezo wa AC Milan Leonardo amethibitisha kuwa klabu hiyo ya Serie A imezungumza Chelsea kuhusu uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati Cesc Fabregas, 31. (London Evening Standard)
Winga wa Bayern Munich Mholanzi Arjen Robben, 34, anasema atastaafu ikiwa ofa ya sasa haitafanikiwa wakati mkataba wake utamalizika msimu huu.
via: Bbc
Social Plugin