Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBA NA MTIBWA ZAPEWA ONYO NA TFF UGENINI

Mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka nchini (TFF), Ammy Ninje amevikumbusha vilabu vinavyoiwakilisha Tanzania kimataifa, Simba na Mtibwa Sugar kuwa vijiepushe na vitendo vya hujuma nje ya uwanja katika mechi zao za ugenini.

Ninje amesema ana imani na vilabu hivyo kuwa vimejiandaa vya kutosha na wao kama TFF wanaamini mechi zao za ugenini zitakuwa za kiungwana na watafuatilia kila hatua kuhakikisha vilabu vyao vinatendewa haki.

''Tunaamini wachezaji wana uzoefu na watafuata kile walimu watakachowaambia na hawataathiriwa na mambo ya nje ya uwanja kama ambavyo huwa inatokea kwenye mechi nyingi za ugenini'', amesema Ninje.

Aidha Ninje amesisitiza kuwa shirikisho linaamini katika 'Fair Play' na dunia ya soka inataka hivyo kwahiyo Simba na Mtibwa hawatakiwi kuyumbishwa na propaganda za nje ya uwanja.

Simba leo watakuwa jijini Manzini, eSwatini kukipiga na wenyeji wao Mbabane Swallows wakati Mtibwa Sugar wao wapo jijini Victoria huko Seychelles ambapo kesho watakipiga na wenyeji wao Northen Dynamo.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com