Uongozi wa Clouds Media Group, umetangaza kuwa tamasha la Fiesta ambalo liliahirishwa kufanyika Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Oktoba, litarudiwa tena mwezi huu.
Taarifa hizo za kurudiwa kwa tamasha hilo, zimethibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga kupitia kipindi cha Clouds 360.
Novemba 24, 2018 manispaa ya Kinondoni ilieleza kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa walio karibu na eneo la Leaders Club lilipopangwa kufanyika Fiesta, kuwataka waandaaji kulihamishia tamasha hilo viwanja vya Tanganyika Peakers.
Baada ya uamuzi huo wa manispaa, waandaaji wa tamasha hilo walitangaza kuwa halitafanyika tena.
“Wakati mwingine matatizo huibua fursa kubwa na bora zaidi. Tamasha lijalo litakuwa kubwa kuliko lile la awali, wale ambao walikuja kutoka mikoani kwa ajili ya kuhudhuria shoo hiyo tutaangalia namna ya kuwapunguzia machungu kwenye tamasha hilo,” amesema Kusaga.
Amesema kutokana na kutofanyika kwa tamasha hilo amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuangalia namna bora ya kulifanya tamasha hilo.
Social Plugin