Jarida la uchumi duniani limetoa taarifa kuwa itachukua miaka 200 kufikia usawa wa malipo kati ya mwanamke na mwanaume
Ripoti ya mwaka 2018 toleo la uwiano wa kijinsia ulimwenguni, lililoandaliwa na Jukwaa la uchumi duniani (WRF) na kutolewa tarehe 17 mwezi Desemba limeweka picha halisi ya hali ya haki za wanawake katika siasa, uchumi na elimu.
Wakati ripoti hiyo imeandika kuwa nchi 88 kati ya 149 zilizo fanyiwa utafiti zimeonyesha kuongeza juhudi katika kushughulikia maswala ya usawa wa malipo na uwakilishi wa kisiasa lakini picha halisi ya matokeo kwa ujumla bado ni changamoto. Ina kadiriwa kuwa kufikia usawa wa kijinsia ulimwenguni itachukua miaka 100.
Hata hivyo hiyo ni taarifa njema ukifananisha na na hali ilivyo katika baadhi ya maeneo kama inavyo onekana hapa chini.
1. Miongo miwili mpaka kufikia usawa wa malipo
Kukosekana kwa usawa katika ushirikiano wa kiuchumi na fursa duniani kote inaweza kuwa jambo la wazi kabisa, lakini kutokuwa na usawa wa kijinsia katika maswala ya kisiasa ni tatizo kubwa zaidi.
Japokuwa pengo la kisiasa linaondoka haraka zaidi.
Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kazi la kimataifa (ILO) inasema utofauti wa kipato ulimwenguni kati ya mwanamke na mwanaume unakaribia asilimia 20.
Shririka la WEF pia lilifafanua kuwa wanawake wataendelea kufanya shughuli zisizo na malipo.
"Kati ya nchi 29 ambazo takwimu zake zipo, wanawake wanatumia mara mbili zaidi ya muda wao katika kazi za nyumbani na shughuli nyingine zisizo na malipo tofauti na wanaume," ripoti hiyo imeelezaa.
Pia watafiti wamegundua asilimia 60 ya nchi zilizofanyiwa tafiti wanawake wana fursa sawa ya kupata huduma za kifedha kama wanaume, huku umiliki wa ardhi ukiwa asilimia 42.Zaidi ya asilimia 60 ya wabunge Rwanda ni wanawake lakini kiujumla wanawake wabunge duniani ni asilimia 24 tu.
2. Fursa katika ofisi za umma.
Kwa sasa wanawake ambao ni wakuu wa nchi wapo katika nchi 17 kati ya 149 zilizo fanyiwa uchambuzi katika ripoti ya kijinsia ulimwenguni, ni zaidi ya asilimia 11.
"Kwa miaka 50 iliyopita, wastani wa wanawake ambao ni wakuu wa nchi au mawaziri wakuu katika nchi hizo 149 walikaa madarakani kwa wastani wa miaka miwili," taarifa imefafanua.
Hali ni ya ahueni katika nafasi za uwaziri, kukiwa na asilimia 18 ya mawaziri wanawake duniani.
Katika bunge kuna asilimia 24 tu ya wanawake.
Moja ya nchi ambazo zimefanya vizuri ni Rwanda ambapo ulimwengu mzima ndio nchi yenye usawa mkubwa kabisa wa wanawake bungeni kwa asilimia 61.3Pengo la usawa wa kijinsia katika elimu litazibwa katika kipindi cha miaka 14 kwa mujibu wa WEF
3. Vikwazo vya elimu bado vikubwa katika baadhi ya nchi
Kwa mujibu wa WEF, nchi 44 zimeonyesha kuwa na wanawake wasiojua kusoma na kuandika ni asilimia 20.
Nchi ambayo imefanya vibaya zaidi ni Chad, ambapo kuna asilimia 13 pekee ya wanawake wanaojua kusoma na kuandika.
Japo kuwa ukosefu wa usawa wa kijinia katika elimu ulimwenguni unaweza kuondolewa ndani ya miaka 14, haraka zaidi ya ilivyo tazamiwa awali.
Lakini bado kuna wasiwasi katika takwimu za jumla za wanafunzi wanao jiunga shule: Wasichana asilimia 65 na wavulana asilimia 66 wamejiunga elimu ya sekondari ulimwenguni.a
4. Usawa wa kiafya
Ripoti hiyo inaeleza kuwa usawa wa kijinsia katika afya ulimwenguni unakaribia kutimia.
Kipengele hicho kimeangazia muda wa kuishi na upatikanaji wa huduma za afya.
Katika nchi zote zilizo chunguzwa, ninchi tatu pekee Kuwait, Bhutan na Bahran wanawake wanaishi muda mrefu zaidi kama wanaume.Iceland kwa mara nyingine ndio nchi yenye usawa wa kijinsia zaidi ya nchi zote duniani
5. Pesa pekee haimalizi utofauti wa kijinsia
Wakati nchi nne zilizo endelea - Iceland, Norway, Sweden and Finland - zikiongoza kipengele cha utofauti katika jinsia, listi hiyo haija ongozwa na nchi tajiri kama unavyofikiria.
Nicaragua (5), Rwanda (6), Philippines (8), na Namibia (10) ndio nchi zinazo endelea katika 10 bora na nchi hizi zinazo endelea ndio zimefikisha karibu nusu ya 30 bora.
Nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani - Amerika - ipo nafasi ya 51, wakati Italia ipo nafasi ya 70.
Nchi nyingine ambazo hazikutegemewa kushika nafasi ya chini ni Russia (75th), Brazil (95), China (103) na Japan (110)
Chanzo:Bbc
Social Plugin