Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Desemba 1,2018 imeungana na wadau mbalimbali ulimwenguni kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya ‘Pima,Jitambue,Ishi’ alikuwa Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko.
Maadhimisho hayo yaliyoambatana na upimaji Virusi vya UKIMWI kwa wananchi yameenda sanjari na Uzinduzi Kampeni ya Utoaji Chanjo ya Matone ya Vitamini A na Minyoo kwa watoto wenye umri wa miezi sita hadi miaka mitano.
Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga inatekeleza shughuli za VVU na UKIMWI kwa kushirikiana na wadau wa UKIMWI wakiwemo CUAM,JHPIEGO,TVMC,MECEG,Rafiki SDO,AGAPE,Thubutu Africa,YAWE,AGPAHI,SHIDEPHA na USAID Tulonge Afya.
Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha 35 za matukio yaliyojiri….Tazama picha hapa chini
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani halmashauri ya wilaya ya Shinyanga katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza,Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko.Aliwahamasisha wananchi kujitokeza kupima afya zao ili kubaini kama wana maambukizi ya VVU au la, na wanapobaini kuwa wana maambukizi basi waanze kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Thomas Tukay akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1,2018.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngasa Mboje akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1,2018.
Madiwani wa CCM katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Jumanne Katundu akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Desemba 1,2018.
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Dkt. Amos Mwenda akitoa taarifa kuhusu hali ya maambukizi ya VVU katika halmashauri hiyo.
Raphael Sabuni akitoa ushuhuda jinsi alivyoishi na VVU tangu mwaka 2007 yeye na mkewe kwa kuzingatia matumizi sahihi ya ARV,s na kuwashauri wananchi kujitokeza kupima afya zao.
Maadhimisho yanaendelea.
Wadau wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wa UKIMWI wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Sungu sungu wakiendelea kuonesha makeke yao.
Burudani ya Ngoma ya zeze ikiendelea.
Kikundi cha Mabulo ya Jeshi kinachosimamiwa na shirika la TVMC kikitoa burudani ya wimbo.
Kikundi cha Mabulo ya Jeshi kinachosimamiwa na shirika la TVMC kikitoa burudani.
Maadhimisho yakiendelea.
Burudani ya ngoma ya kadete ikiendelea.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani halmashauri ya wilaya ya Shinyanga katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza,Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akielekea kwenye mabanda yaliyokuwa yanatoa huduma ya upimaji VVU katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akiingia katika banda la kupima VVU la JHPIEGO.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akiuliza taratibu za upimaji VVU ndani ya banda la kupima VVU la JHPIEGO.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akiwa ndani ya banda la JHPIEGO.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akipewa ushauri nasaha ndani ya banda la kupima VVU la JHPIEGO.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akipima uzito katika banda la JHPIEGO kabla ya kupima VVU.
Akina mama wakiwa kwenye foleni wakisubiri huduma ya kupima VVU.
Wanaume wakisubiri huduma ya kupima VVU kwenye banda la JHPIEGO.
Akina mama wa Pandagichiza wakiimba wimbo wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Desemba 1,2018.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akimpa mtoto matone ya Vitamin A wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Utoaji Chanjo ya Matone ya Vitamini A na Minyoo kwa watoto wenye umri wa miezi sita hadi miaka mitano.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akimpa mtoto matone ya Vitamin A wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Utoaji Chanjo ya Matone ya Vitamini A na Minyoo.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akimwangalia mtoto baada ya kumpa matone ya Vitamin A wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Utoaji Chanjo ya Matone ya Vitamini A na Minyoo.
Uzinduzi wa Kampeni ya Utoaji Chanjo ya Matone ya Vitamini A na Minyoo kwa watoto wenye umri wa miezi sita hadi miaka mitano ukiendelea.
Wanafunzi wa shule ya msingi Shilabela wakiimba kwaya.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akitoa zawadi ya madaftari na kalamu kwa mwanafunzi wa shule ya msingi.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akitoa zawadi ya sare za shule kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Pandagichiza zilizotolewa na shirika la AGAPE.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akitoa zawadi ya sare za shule kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Pandagichiza zilizotolewa na shirika la AGAPE.
Wadau wa UKIMWI wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Desemba 1,2018.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin