Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Jaji mstaafu, Steven Bwana kuwa mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa imesema kuwa, pamoja na uteuzi huo, Rais amewateua makamishna watano wa tume ya utumishi wa umma.
Walioteuliwa ni; "George D. Yambesi, Balozi mstaafu John Michael Haule, Immaculate Ngwale, Yahya Mbila na Balozi mstaafu Daniel Ole Njolay".
Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Novemba 22.
Social Plugin