Muigizaji maarufu nchini Kenya, Jamal Nasoor maarufu (Baba Junior) aliyejipatia umaarufu kupitia mchezo wa kuigiza runingani wa Vioja Mahakamani akicheza kama Hakimu, ameuwawa na mpenzi wake anayetambulika kwa jina la Grace Kanamu.
Kifo cha Jamal ambaye ametamba pia katika tamthilia ya Junior iliyokuwa ikionyeshwa kupitia Televisheni ya KTN, kinaripotiwa kutokea Jumanne Desemba 11 baada ya kutokea majibishano kati yake na mpenzi wake huyo waliopokuwa katika sherehe iliyofanyika katika klabu moja ya usiku hoteli ya Arks.
Imeelezwa kuwa baada ya majibishano hayo Grace alichukua kisu na kumchoma Jamal na kusababisha kifo chake.
Baada ya kuchomwa kisu Jamal alikimbizwa katika hospitali ya Shalom lakini jana Desemba 12 alifariki dunia, Polisi wamesema bado wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.
Aidha inasemekana Jamal na Grace walikuwa majirani katika eneo walilokuwa wanaishi la Syokimau katika kaunti ya Machakos na walianza kuwa na uhusiano uliodumu kwa miezi Tisa baada ya wote wawili kutalikiana na wenza wao.
Social Plugin